13 Julai 2020 - 09:47
Televisheni ya Saudia yaeneza uongo na kuendesha propanda chafu dhidi ya Wapalestina

Wizara ya Mambo ya Ndani ya serikali ya Ukanda wa Ghaza imeilalamikia vikali televisheni ya Saudi Arabia ya al Arabia kwa kueneza uongo na propaganda chafu dhidi ya Wapalestina na imekanusha madai ya uongo ya televisheni hiyo iliyodai kuwa baadhi ya makamanda wa muqawama wa Palestina wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuufanyia ujasusi utawala wa Kizayuni wa Israel.

Shirika la habari la ABNA24 limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya serikali ya Ghaza imekanusha madai ya televisheni hiyo ya Saudi Arabia na kusema kuwa televisheni ya al Arabia ni chombo cha ukoo wa Aal Saud cha kuendesha propaganda chafu dhidi ya Wapalestina na kupotosha walimwengu kuhusu kadhia ya Palestina.

Televisheni ya al Arabia ya Saudi Arabia jana Jumapili ilidai kuwa, makamanda 16 wa Brigedi za Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuufanyia ujasusi utawala wa Kizayuni wa Israel.

Hadi hivi sasa viongozi wa kisiasa na kiutamaduni wa Palestina wamekuwa wakiilaani vikali televisheni hiyo ya Saudia kwa kushirikiana na utawala wa Kizayuni kuendesha propaganda chafu dhidi ya Wapalestina. Kiujumla televisheni hiyo muda wote inaendesha propaganda za kuusafisha utawala wa Kizayuni ambao unafanya jinai kubwa dhidi ya Wapalesitna na ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu.

Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni hususan baada ya kuingia madarakati Mohammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia, uhusiano wa nchi za Kiarabu zinazopakana na Ghuba ya Uajemi kati yao na utawala wa Kizayuni wa Israel umezidi kuwa mkubwa. Saudi Arabia na baadhi ya nchi za Kiarabu ni viranja wa kupigania kuweko uhusiano mzuri baina ya nchi za Kiarabu na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuangamizwa kabisa kadhia ya Palestina ambako ndiko kiliko Kibla cha Kwanza cha Waislamu kinachokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

342/